Plato wa Konstantinopoli

Plato wa Konstantinopoli (au wa Sakkoudion; labda Konstantinopoli, leo nchini Uturuki, 735 hivi - Konstantinopoli, leo nchini Uturuki, 4 Aprili 814) alikuwa abati mwanzilishi wa monasteri ya Mlima Olimpo huko Bitinia baada ya kuacha kazi yake katika ikulu na kukataa uaskofu.

Alitetea sana heshima kwa picha takatifu pamoja na mtoto wa ndugu yake, Theodoro wa Studion, wakati wa dhuluma ya serikali ya Dola la Roma Mashariki na katika mtaguso wa pili wa Nisea. Pamoja naye tena alirekebisha monasteri maarufu ya Studion.[1].

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 4 Aprili[2][3][4].

  1. http://www.santiebeati.it/dettaglio/48475
  2. Martyrologium Romanum
  3. Great Synaxaristes: (Kigiriki) Ὁ Ὅσιος Πλάτων. 4 Απριλίου. ΜΕΓΑΣ ΣΥΝΑΞΑΡΙΣΤΗΣ.
  4. (Kigiriki) Συναξαριστής. 4 Απριλίου Archived 8 Agosti 2022 at the Wayback Machine.. ECCLESIA.GR. (H ΕΚΚΛΗΣΙΑ ΤΗΣ ΕΛΛΑΔΟΣ).

From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Tubidy